• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China atoa salamu za pongezi kwa waziri mkuu mpya wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2019-07-25 19:03:15

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa salamu za pongezi kwa Bw. Boris Johnson kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

    Bw. Li amesema katika miaka ya hivi karibuni, mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uingereza ni mzuri. Wakuu wa pande hizo mbili wamedumisha mawasiliano. Matokeo makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa sekta mbalimbali. Amemsifu Bw. Johnson kujitahidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili alipokuwa meya wa mji wa London na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza.

    Bw. Li pia amesema, China inazingatia maendeleo ya uhusiano kati yake na Uingereza. Na anapenda kushirikiana na Bw. Johnson kuongeza uaminifu wa kisiasa, kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali, kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi zao na kulinda mfumo wa pande nyingi na biashara huria ili kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa dunia unaofungua mlango.

    Wakati huohuo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying amesema China inapenda kushirikiana na Uingereza kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Habari zinasema waziri mpya wa Uingereza Bw. Boris Johnson hivi karibuni alipohojiwa na televisheni ya Phonenix ya Hong Kong alisema serikali ya Uingereza itakuwa karibu sana na China, na ina hamu kubwa na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako