• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Sakata la Hisa Simba, wataaalamu watoa ufafanuzi

    (GMT+08:00) 2019-07-26 10:08:22

    Wakati serikali ya Tanzania kupitia waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kueleza namna ambavyo klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam iliyoingia mfumo wa kampuni wa hisa ikieleza jinsi mfumo unavyopaswa kuwa, Dkt. Mwakyembe alisema mfumo wa hisa wa klabu hiyo hauruhusu mwekezaji mmoja kama ambavyo ilikuwa ikifahamika na wengi bilionea Mohamed Dewji ndiye mwekezaji mwenye hisa asilimia 49, huku asilimia zilizosalia zinakuwa za wanachama.

    Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya Orbit , washauri wa uwekezaji kwenye masoko ya mitaji ya hisa Juventus Simon amesema kwakuwa Dewji ni mwekezaji wa mkakati wa klabu hiyo na malengo yake ni kupata faida kutoka kwenye fedha alizoweka, hivyo hayuko tofauti na wawekezaji wengine kwenye sekta zingine za uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako