• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bidco yazindua kiwanda kipya mjini Ruiru

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:26:06
    Serikali ya Kenya ina mipango ya kuendelea kufufua viwanda vingine hapa nchini ili kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.

    Rais Uhuru Kenyatta amesema hivi karibuni viwanda 40 vitafunguliwa kote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kuangazia ajenda nne kuu za serikali.

    Ameyasema hayo Alhamisi wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha Bidco Industrial Park mjini Ruiru. Kiwanda hicho amesema kitaajiri takribani zaidi ya wafanyakazi 5,000 kwa siku za hivi karibuni.

    Amesema atafanya jinsi awezavyo kuona ya kwamba ameangamiza umaskini ambao umekuwa ni tatizo kubwa nchini.

    Aidha, amefafanua ushirikiano wake na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ni jambo muhimu kwa nchi kwa sababu utulivu wa nchi umedhihirika huku biashara zikinawiri kote nchini. Amesema hivi karibuni Kenya itakuwa na maeneo mawili – Eldoret na Juja (JKUAT) – ya kutengeneza vipatakilishi na hiyo itamaanisha Kenya inapiga hatua kubwa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako