• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Onyo kali kwa wanunuzi pamba

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:27:06

    Serikali ya Tanzania imetoa onyo kali kwa wanunuzi wa pamba nchini humo kwa kushindwa kutekeleza makubaliano ambayo waliwekeana na serikali kuhakikisha wananunua pamba yote ambayo bado ipo kwenye maghala. Kauli ya serikali imekuja baada ya kuendelea kuwapo kwa pamba nyingi kwenye maghala hayo, wakati serikali iliwadhamini wanunuzi wote kuchukua fedha benki na kuanza kununua pamba.

    Onyo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, baada ya kutembelea na kujionea pamba ikiwa imehifadhiwa nje ya ghala katika chama cha msingi cha ushirika (Amcos) Zuya Mtaa wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi.

    Mgumba alisema wanunuzi wa pamba walikubaliana na serikali wadhaminiwe ili kukopeshwa na benki, jambo ambalo lilifanyika, lakini anashangaa kwa nini mpaka leo wameshindwa kununua pamba.

    Alisema serikali ilichukua dhamana hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa pamba na fedha ambazo wanunuzi walikopeshwa na benki zinatakiwa kutumika kwa ajili ya kununua pamba tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako