• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni unafiki kwa nchi za magharibi kulaani mfumo wa kutathmini uaminifu wa kijamii wa China

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:34:37

    Gazeti kubwa la Ujerumani la Sddeutsche Zeitung limetoa habari kusema, ni unafiki kwa nchi za magharibi kulaani mfumo wa kutathmini uaminifu wa kijamii wa China.

    Habari hizo zimesema, uchunguzi kamili katika nchi hizo unaendelea kwa siri na data za umma zimekusanywa kwa wingi. Wabunge wa nchi za magharibi wanapaswa kuchukua hatua kuzuia kitendo hicho.

    Habari hizo pia zimesema, kwa mujibu wa uchunguzi wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon kwa tovuti zaidi ya elfu 20, asilimia 93 ya kapampuni za uendeshaji wa tovuti zimeshirikiana na upande wa tatu kutumia pamoja data za watumiaji, hasa makampuni makubwa yakiwemo Google na Facebook.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako