• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shambulizi la hospitali ya muda ya Tripoli lasababisha vifo vya wanyakazi wa afya watano na wengine wanane kujeruhiwa

    (GMT+08:00) 2019-07-28 17:45:23

    Hospitali ya muda mjini Tripoli ililipuliwa kwa mabomu jana, ambapo wafanyakazi watano wa afya waliuawa na wengine wanane kujeruhiwa, huku mapambano kati ya vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na jeshi la mashariki yakiendelea.

    Kwenye taarifa yake wizara ya afya ya nchi hiyo imelaani vikali shambulio hilo na kuzingatia kuwa mashambulizi hayo mabaya na yanayojirejea pamoja na vurugu tangu kuanza kwa vita dhidi ya mji wa Tripoli yanakiuka mikataba na sheria za ndani na za kimataifa za ubinadamu ambazo zinasema ni kosa la jinai kuwalenga wafanyakazi wa afya.

    Toka mwezi Aprili jeshi la mashariki linaloongozwa na jenerali Khalifa Haftar lilianzisha mapigano linalolenga kudhibiti Tripoli kutoka kwa serikali. Kulingana na Shirika la afya duniani WHO, mapigano hayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja, na wengine zaidi ya 5,700 kujeruhiwa, na kuwalazimisha zaidi ya watu laki moja na ishirini kukimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako