• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Michuano ya kombe la Victoria- Kenya yaifanya Zambia kitoweo

    (GMT+08:00) 2019-07-29 08:47:37
    Timu za raga za Kenya na Zimbabwe zimepata ushindi ugenini kwenye michezo yao ya raga ya wachezaji 15 kila upande katika michuano ya kombe la Victoria iliyopigwa mwishoni mwa wiki.

    Kenya ilicheza na Zambia na kushinda kwa alama 43-23 mjini Kitwe Zambia, nao Zimbabwe walikuwa mjini Kampala Uganda na kuizamisha Uganda kwenye ardhi yao ya nyumbani kwa alama 31-26.

    Kenya itaelekea Zimbabwe kumenyana na wenyeji hao Agosti 3, huku Agosti 10, Uganda watakipiga na Zambia jijini Kampala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako