• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Derby ya Afrika Mashariki- Tanzania na Kenya zatoshana nguvu, zatoka sare 0-0

    (GMT+08:00) 2019-07-29 08:47:40
    Baada ya kucheza katika michuano ya AFCON iliyomalizika mwezi huu nchini Misri, jana majirani wawili Taifa Stars ya Tanzania waliwakaribisha Harambee Stars ya Kenya uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya fainali ya CHAN 2020.

    Kipindi cha kwanza timu zote mbili hazikupiga shuti lililolenga lango la mpinzani wake.

    Naye kocha wa Harambee Stars amesema, licha ya kikosi chake kuwa kipya lakini vijana wake wamecheza vizuri lakini hawakuwa makini katika umaliziaji hali iliyopeleka kushindwa kupata hata goli moja, ameshaona mapungufu na atayafanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano

    Taifa Stars italazimika kushinda ugenini jijini Nairobi nchini Kenya kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Agosti 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako