• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Wakati usajili ukiendelea, ndugu wawili kukinukisha Bucks

    (GMT+08:00) 2019-07-29 08:47:40
    Usajili unaendelea ikiwa ni maandalizi ya ligi ya kikapu ya Marekani (NBA) kuelekea msimu ujao baadaye mwaka huu ambapo kila timu inaendelea kuongeza na kupunguza wachezaji wao ili kuimarisha vikosi kwa lengo la kufanya msimu uwe bora na wa ushindani zaidi.

    Dili jipya limefanyika Milwaukee Bucks ambayo imemtoa Thanasis Antetokounmpo nchini Ugiriki akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya ligi ya kikapu ya nchini kwao. Meneja wa Bucks, Jon Horst amemtangaza mchezaji huyo kuwa ataongeza nguvu kwenye timu hiyo kulingana na alichokitaja kuwa mzoefu na mwenye uwezo wa kushindana. Thanasisi ataungana na kaka yake Giannis ambaye ni MVP wa msimu uliopita kukipiga katika timu hiyo ya Milwaukee Bucks.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako