• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaanza tena kununua mazao ya kilimo ya Marekani

  (GMT+08:00) 2019-07-29 08:59:32

  Mamilioni ya tani za soya za Marekani zimepakiwa kwenye meli tayari kusafirishwa nchini China, ikiwa ni baada ya mkutano wa marais wa nchi hizo mbili uliofanyika mjini Osaka, Japan.

  Wakati huohuo, Marekani imetangaza kufuta ongezeko la ushuru kwa aina 110 za bidhaa za viwandani za China, na kusema inapenda kuhimiza kampuni za teknolojia za juu za Marekani kuendelea kuuza bidhaa kwa kampuni za China.

  Tangu tarehe 19 Julai, baadhi ya kampuni za China zilianza kuuliza bei ya mazao ya Marekani ikiwemo Soya, na pamba, na kutoa oda kadhaa, pia kampuni hizo zimetoa ombi la kusamehe ushuru ulioongezeka wa bidhaa hizi za Marekani kwa serikali ya China.

  China imeitaka Marekani kuchukua hatua halisi za kutekeleza ahadi yake, ili kutoa mazingira mazuri kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako