• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuu ya China yawataka watu wa Hong Kong kupinga kithabiti mabavu

    (GMT+08:00) 2019-07-29 18:40:28

    Msemaji wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macau ya baraza la serikali la China Bw. Yang Guang, leo hapa Beijing amesema maendeleo ya hali ya Hong Kong, hasa vitendo vya kimabavu vilivyofanywa na baadhi ya watu wenye msimamo mkali, vimeathiri vibaya hali ya ujumla ya ustawi na utulivu ya Hong Kong, na kuwataka watu wa sekta mbalimbali za jamii mkoani Hong Kong kupinga kithabiti mabavu.

    Bw. Yang amesema maendeleo ya mabavu yaliyotokea katika Hong Kong yameharibu vibaya utawala wa sheria na utaratibu wa jamii, kutishia vibaya usalama wa mali na maisha ya wakazi wa Hong Kong, na kugusa mpaka wa mwisho wa sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili", ambayo hayawezi kuvumiliwa. Jamii yoyote yenye ustaarabu na utawala wa sheria haiwezi kuvumilia kutokea mara kwa mara kwa vitendo vya mabavu.

    Amewataka wakazi wa Hong Kong kutambua ubaya wa hali ya hivi sasa, na kupambana kwa pamoja na mabavu na uhalifu uliofanywa na watu wenye msimamo mkali na kuwazuia kuendelea kuiharibu Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako