• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maafisa kutoka Uganda wakamata Wavuvi 30 wa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-07-29 19:23:22
    Wavuvi 30 wa Kenya wanasemekana kuwekwa kizuizini nchini Uganda baada ya kukamatwa wakati wakivua samaki katika Ziwa Victoria.

    Wavuvi hao wanasemekana waliwekwa kizuizini katika Kisiwa cha Hama baada ya kukamatwa na maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA).

    Haijulikani ni kwanini walipelekwa katika kisiwa hicho lakini Maafisa wa Kitengo cha Usimamizi wa Bahari (BMU) katika Kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya, wanaamini wavuvi wanaweza kuwa walivuka mpaka wa kati ya Kenya na Uganda kiharamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako