• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Madrid wasitisha dili la Bale kuelekea China

    (GMT+08:00) 2019-07-30 07:44:38
    Uhamisho wa winga wa Real Madrid kuelekea China umefutwa na sasa winga huyo wa Wales anatarajia kuendelea kuwepo Real Madrid.

    Bale mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kujiunga na klabu ya China Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu kwa dau la pauni milioni 1 kwa wiki.

    Wiki iliopita meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane alisema Bale alikuwa anakaribia kuondoka Madrid baada ya kiwango chake cha mchezo kuzorota. kwa sasa mchezaji huyo hana maelewano mazuri na Zidane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako