• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi zaidi 50 zaunga mkono msimamo wa China juu ya suala la mkoa wa Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-07-30 08:28:12

    Mabalozi wa nchi zaidi ya 50 wamemwandikia barua ya pamoja mwenyekiti wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na kamishna mwandamizi wa haki za binadamu, wakiunga mkono msimamo wa China juu ya masuala yanayohusiana na mkoa wa Xinjiang.

    Akiongea kwenye mkutano na wanahabari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, hivi sasa suala la mkoa wa Xinjiang ni la kuondoa ugaidi na itikadi kali, na wala sio suala la dini na haki za binadamu. Amesema serikali ya mkoa wa Xinjiang imechukua hatua madhubuti za kupambana na ugaidi na itikadi kali kwa mujibu wa sheria, juhudi hizo zimeimarisha kidhahiri usalama katika mkoa huo, ambao kwa miaka mitatu mfululizo haukushuhudia matukio ya kigaidi.

    Bi. Hua Chunying amesisitiza kuwa China inajitahidi kushirikiana na pande mbalimbali katika kuyahimiza mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa kufuata kwa makini kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kushughulikia masuala ya haki za binadamu kwa haki na bila upendeleo, na kuhimiza maendeleo ya shughuli za haki za binadamu za kimataifa kwa njia ya ushirikiano na mazungumzo ya kiujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako