• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana wakumbatia ukulima wa shamba kitalu

    (GMT+08:00) 2019-07-30 18:39:55
    Licha ya kuwa sekta ya kilimo imezidi kuimarika sana barani Afrika kwa miaka mingi, bado mataifa mengi yanazidi kutegemea chakula cha kuagizwa kutoka mataifa yaliyostawi. Kadri miaka inavyokwenda, ndivyo idadi ya watu barani. Inakisiwa kwamba Afrika itakuwa na watu bilioni 2 ifikapo mwaka wa 20150, idadi ambayo itategemea sana sekta ya kilimo.

    Tayari, vijana kutoka taifa la Rwanda wameanza kutumia teknolojia ya kisasa kwenye kilimo cha shamba kitalu almaarufuu green house. Wengi wameanza kuasi mitindo ya kilimo cha zamani na kukumbatia kilimo kinachotumia teknolojia ya kisasa. Tayari, mazao yameanza kushuhudiwa. Wito umezidi kutolewa kwa vijana nchini Rwanda kuanza kilimo cha shamba kitalu kama njia moja ya kujiajiri, kando na kuzalisha vyakula aina mbali mbali kwa taifa la Rwanda na mataifa mengine.

    Mojawapo ya manufaa ya shamba kitalu ni kwamba, mkulima ana nafasi ya kupanda mazao yake msimu wowote mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako