• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuuza mafuta yake ng'ambo

    (GMT+08:00) 2019-07-30 18:40:18

    Kampuni ya uchimbaji mafuta ya Tullow Oil imesema, kiwango cha mafuta kutoka Turkana kilichofikishwa Mombasa kwa uhifadhi, sasa kimetosha kusafirishwa kwa meli hadi nchi ya kigeni kwa majaribio ya kibiashara.

    Mpango huo unatarajiwa kufanikishwa kabla robo hii ya tatu ya mwaka ikamilike, ifikapo mwezi Septemba, ingawa haijajulikana wazi mafuta yanasafirishwa hadi nchi gani.

    Kwenye ripoti ya kibiashara iliyotumwa kwa wanahabari, Tullow ilisema kufikia sasa mapipa 200,000 ya mafuta ambayo ni sawa na lita 31.8 milioni yamehifadhiwa Mombasa. Tullow ilisema hatua kubwa zilizopigwa sasa zimeleta matumaini kwamba, Kenya itaanza rasmi biashara ya uuzaji mafuta kati ya Julai na Desemba mwaka ujao. Usafirishaji mafuta kutoka Turkana ulikumbwa na vikwazo tele vilivyopelekea mpango wa serikali kuanzisha shughuli hiyo kabla 2017 kugonga mwamba.

    Rais Uhuru Kenyatta alizindua usafirishaji kutoka Turkana hadi Mombasa mwaka uliopita, lakini kukawa bado na changamoto hasa kuhusu usalama, miundomsingi na maelewano ya ugavi wa mapato ya rasilimali hiyo kati ya serikali kuu, za kaunti na jamii za maeneo ambako mafuta yanachimbwa.

    Tullow jana ilisema mashauriano kuhusu masuala ya kifedha yalikamilika na kupitishwa mnamo Juni 25 mwaka huu, hatua ambayo ilitia moyo kuendeleza mbele mradi huo utakaoingiza Kenya kwenye orodha ya mataifa Afrika yanayojiletea mapato kutoka kwa uuzaji mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako