• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mechi ya marudiano na Tanzania itakuwa ngumu –Migne

    (GMT+08:00) 2019-07-31 08:11:05
    Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Sebastian Migne ameweka wazi kuwa mchezo wa marudiano baina ya Harambee Stars na timu ya taifa ya (Tanzania Taifa Stars) itakayopigwa jumamosi ya wikiendi hii jijini Nairobi itakuwa ngumu kwa pande zote mbili.

    Jumapili mwishoni mwa wikiendi, timu hizo zilicheza mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya bila kufungana mchezo wa kuwania kufuzu fainali za CHAN kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

    Migne amesema, mechi ya kwanza ingemalizika kwa suluhu ya kufungana mabao ingekuwa nafuu kwao kuliko ya bila kufungana.

    Nao wachezaji wa Tanzania wamesema wanakwenda Kenya kutafuta ushindi baada ya kuukosa nyumbani kwao Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako