• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asisitiza kuweka mkazo katika mageuzi ili kuimarisha jeshi

  (GMT+08:00) 2019-08-01 08:27:54

  Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Xi Jinping, amesisitiza kuongeza juhudi za kutekeleza mkakati wa kuimarisha jeshi kupitia mageuzi, ili kuendeleza shughuli za kujenga jeshi lenye nguvu katika zama mpya.

  Rais Xi amesema hayo alipoongoza kikao cha Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya CPC kuhusu mageuzi ya sera na taasisi za kijeshi kilichofanyika jana.

  Kwenye kikao hicho kilichofanyika kabla ya Siku ya Jeshi la China ambayo ni Agosti Mosi kila mwaka, Rais Xi ametoa salamu kwa wanajeshi wote wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China PLA, askari polisi, wanamgambo na kikosi cha akiba kwa niaba ya Kamati kuu ya Chama cha CPC na Kamisheni kuu ya jeshi.

  Rais Xi amesema mageuzi ya sera na taasisi za kijeshi yanalenga kutatua tatizo la sera zilizopo kutoendana na mahitaji ya zama mpya, majukumu mapya na taasisi mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako