• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATE yafanya mkutano na wafanyabiashara wa China

    (GMT+08:00) 2019-08-01 19:20:16
    Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China nchini Tanznaia na Chama cha Waajiri nchini Tanzania ,jana walifanya mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji nchini Tanzania kwa wafanyabiashara kutoka nchini humo na changamoto za kibiashara wanazokutana nazo katika uwekezaji wao.

    Mkutano huo umejumuisha wadau mbalimbali kutoka kituo cha Taifa cha Uwekezaji,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Idara ya Uhamiaji,Ofisi ya Kamishna wa kazi,na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).

    Akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),Dkt Aggrey Mlimuka,alisema kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine nchini Tanzania,Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China bado wameendelea kukumbana na changamoto nyingi zinazohusiana na uwekezaji ,masuala ya kodi,utekelezaji wa sheria za kazi na ajira,ajira za wafanyakazi,mikataba,taratibu za usitishwaji wa mikataba,vibali vya kufanya kazi kwa wageni a nyingine nyingi.

    Alisema wao kama ATE kwa kushirikiana na wadau wao wameona ni vyema kuandaa mkutano huo ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.

    Aidha Dkt Mlimuka alitoa wito kwa serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini humo ili kuwavutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako