• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yafungua sekta ya benki kwa raia wanaoishi nje ya nchi,na walio na uraia wa nchi mbili

    (GMT+08:00) 2019-08-01 19:21:59
    Bunge la Ethiopia jana lilipitisha mswada wa kufungua sekta ya fedha nchini humo kwa raia takriban milioni 5 wanaoishi nje ya nchi au wale walio na uraia wan chi mbili,ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu kununua hisa katika benki za ndani na kuanza biashara za kukopesha.

    Mabadiliko hayo ni sehemu ya mabadiliko ya kiuchumi yaliyoanzishwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed wakati alipochukua mamlaka mwaka jana,yanayolenga kupiga jeki hifadhi za mabadilishano ya fedha kigeni,ambayo yalikuwa yameshuka.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mapato,Bajeti na Fedha,Lemlem Hadgo alisema sheria hiyo mpya itawawezesha wazawa wa Ethiopia ambao wanaishi nchi za nje kushiriki katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako