• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-01 19:22:10

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo huko Bangkok amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo.

    Bw. Wang amesema, mkutano kati ya marais wa nchi hizo mbili uliofanyika mwezi wa Juni huko Osaka, Japan, ulifikia makubaliano katika sekta nyingi, ambayo yanaweka bayana mwelekeo wa uhusiano kati ya China na Marekani. Kipaumbele kwa sasa ni kwamba Marekani inapaswa kwenda kwa upande mmoja na China, kutekeleza kihalisi makubaliano yaliyofikiwa na marais hao, kudhibiti migongano juu ya msingi wa kuheshimiana, kupanua ushirikiano katika msingi wa kunufaishana, ili kuhimiza uhusiano huo wenye uratibu, ushirikiano na utulivu.

    Bw. Pompeo amesema anataka kusisitiza tena kuwa rais Donald Trump na serikali ya Marekani hawataki kuzuia maendeleo ya China, na wanapenda kuanzisha ushirikiano na China katika sekta mbalimbali, huku akitumai mazungumzo ya biashara kati ya Marekani na China kupata maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako