• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kilimo yakamilika na wito wa wakulim akukumbatia teknolojia

    (GMT+08:00) 2019-08-01 19:22:19
    Katibu wa kudumu katika Wizara ya Kilimo,na Rasilimali ya Wanayama nchini Rwanda, Jean Claude Musabyimana ametoa wito kwa wanyarwanda,haswa wale walio katika sekta ya kilimo,kukumbatia teknolojia,jambo alilosema litabadilisha maisha yao.

    Huu ndio ujumbe aliutoa kwa wadau mbalimbali wakati akifunga rasmi makala ya 14 ya maonesho ya kila mwaka ya kilimo katika kiwanja cha maonesho cha Mulindi katika wilaya ya Gasabo.

    Kutokana na kuwa kilimo ndio kinachoingiza mapato mengi sio tu kwa wanyarwanda bali pia kwa uchumi wa nchi,mengi yamefanywa ili kuboresha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mpango wa kimkakati ambao utaenda kwa muda wa miaka sita (2018-2024).

    Mpango wa kimkakati kwa ajili ya sekta ya kilimo unalenga kuwaondoa wakulima kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo cha biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako