• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa fedha wakutana Ghana kwa mkutano kuhusu ukuaji wa uchumi Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-02 18:43:27

    Mkutano unaowaleta pamoja mawaziri wa fedha na magavana wa benki barani Afrika unaendelea hivi sasa nchini Ghana ambao kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kufanikisha uwezo wa kitaasisi na uvumbuzi wa kifedha kwa ukuaji endelevu". Mkutano huo ambao ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1963 ukiwa na lengo la kupiga jeki maendeleo barani Afrika.Akizungumza kuhusui mkutano huo, waziri wa fedha wa Uganda Bw Matia Kasaija amesema analenga kubadilishana mawazo na mawaziri wenzake wa Afrika kuhusu maoni ya Benki ya dunia kuhusu maendeleo Afrika.Amesema bara la Afrika linatakiwa kukumbatia uvumbuzi wa kifedha ikiwa linataka kupata mafanikio ya haraka. Kuhusu kauli mbiu ya mkutano huo, benki ya dunia imesema mkutanoi huo utaweka maono ambayo yataleta mabadiliko barani Afrika na kuchangia ukuaji wa uchumi haraka iwezekanavyo katika bara la Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako