• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hoteli ya DusitD2 yafunguliwa baada ya zaidi ya miezi sita

    (GMT+08:00) 2019-08-02 18:43:48
    Hoteli ya DusitD2 iliyoko Riverside Drive, Westlands, Nairobi imefunguliwa baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi sita tangu shambulizi la kigaidi la Januari 15, 2019, katika DusitD2 Complex lililosababisha vifo vya watu 21.

    Sherehe za ufunguzi zimeshuhudia kupandishwa bendera tatu na mwanariadha nguli David Rudisha na mkuu wa hoteli hiyo yenye matawi mbalimbali.

    Hoteli hiyo ambayo imekuwa ikikarabatiwa inamilikiwa na raia wa Thailand ilisalia imefungwa tangu tukio la shambulizi la kigaidi ambalo kundi la al-Shabaab lilikiri kuhusika.

    Hoteli hiyo ambayo imekodisha asilimia kubwa ya vyumba vilivyoko 14 Riverside Complex ilisalia imefungwa licha ya afisi za biashara nyinginezo kufunguliwa.

    Wateja walianza kupata huduma katika hoteli hiyo siku ya Alhamisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako