• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Korea Kaskazini aongoza tena majaribio ya roketi mpya

    (GMT+08:00) 2019-08-03 18:06:21

    Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limetangaza kuwa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mapema jana aliongoza tena majaribio ya mfumo mpya wa roketi ambao ni mkubwa zaidi.

    Shirika hilo pia limesema majaribio yalikuwa ni ya kuridhisha na kukidhi udhibiti wa kimo cha kuruka, uwezo wa kufuatilia na kubadilisha njia, usahihi wa kulenga shabaha na nguvu ya kulipuka ya kichwa cha kombora linaloongozwa. Bw. Kim ameripotiwa kuridhishwa na matokeo ya jaribio hilo.

    Jumatano iliyopita Bw. Kim aliongoza jaribio lingine, na kusema mfumo huo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa mapambano wa jeshi la nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako