• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi wa UNICEF atoa mwito wa kulindwa kwa watoto kwenye maeneo ya migogoro.

    (GMT+08:00) 2019-08-03 18:06:40

    Mjumbe maalum wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Afrika UNICEF anayeshughulika na watoto walioathiriwa na mapambano ya kisilaha Bibi Mariatu Kamara, ametoa mwito wa kuwalinda watoto kwenye maeneo yenye migogoro ya kisilaha.

    Akiongea kwenye mjadala wa wazi kuhusu "watoto kwenye migogoro ya kisilaha" Bibi Mariatu Kamara amesema watoto wengi kama yeye wanaendelea kuonekana kama "maadui na hawatakiwi, au hawakubaliki kwenye jamii zao na hata kwa familia zao" kwenye baadhi ya sehemu za Afrika na sehemu nyingine duniani.

    Bibi Kamara amesema hayo wakati Mkurugenzi wa UNICEF Bibi Henrietha Fora ameutaja mwezi Julai kuwa ni mwezi uliokuwa mbaya zaidi kwa watoto wa mashariki ya kati na Afrika, ambapo mauaji na matendo mengine ya kikatili yametokea kila siku. Amesema nchini Syria watoto 359 wameuawa au kujeruhiwa, na wengine 477 wa Palestina wamejeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako