• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa asema China ni nchi inayoendelea yenye kipato cha kati

    (GMT+08:00) 2019-08-03 18:09:13

    Mkurugenzi wa idara ya utandawazi na mkakati wa maendeleo ya Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Bw. Richard Kozul-Wright amesema si sahihi kuona nchi yenye biashara kubwa ndiyo nchi iliyoendelea, kwani maendeleo yanayohusu uchumi, jamii, mazingira na sekta nyingine nyingi, na China bado ni nchi inayoendelea.

    Bw. Kozul-Wright amesema hayo baada ya serikali ya Marekani kueleza wasiwasi wake na hadhi ya nchi inayoendelea ya China katika Shirika la Biashara Duniani WTO. Amesema nchini China, bado kuna watu milioni 200 wanaoishi kwa kutumia chini dola ya tano kila siku, watu wengi wanaishi vijijini na watu wengi wanakosa ajira tulivu, hali hizo tatu zimeonyesha wazi kuwa China bado ni nchi inayoendelea. Nchi zilizoendelea zimetatua matatizo hayo kwa miongo na hata karne kadhaa zilizopita.

    Bw. Kozul-Wright ameongeza kuwa katika miaka 25 iliyopita, nchi nyingi zimepata maendeleo makubwa ya kiuchumi, lakini pengo la maendeleo kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea bado lipo. Na kuhusu rais Donald Trump wa Marekani kutishia kuchukua hatua ya upande mmoja kama Shirika la Biashara Duniani lisipofanyia mageuzi hadhi ya nchi zinazoendelea, Bw. Kozul-Wright amesema nchi moja mwanachama haina madaraka ya kubadilisha hadhi ya mwanachama mwengine, na dai lake halitaungwa mkono.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako