• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta mbalimbali nchini Marekani zapinga serikali ya Marekani kutishia kuongeza tena ushuru wa bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2019-08-04 17:09:29
    Sekta mbalimbali na vyombo vya habari nchini Marekani vimeeleza kupinga serikali ya Marekani kutishia kuongeza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 300 zinazouzwa nchini humo kuanzia tarehe mosi, Septemba.

    Magazeti makuu ya Marekani ikiwemo The New York Times, yameandika makala yakisema Marekani kutishia kuongeza ushuru tena kwa bidhaa za China kutasababisha kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara duniani, kuleta hasara katika soko la hisa, kupunguza imani ya wawekezaji wa kimataifa na kupunguza ukuaji wa uchumi.

    Shirika la habari la Bloomberg limeonya kuwa baada ya China na Marekani kuanzisha upya mazungumzo yao ya kibiashara huko Shanghai na kukubaliana kukutana tena mwezi ujao, hatua hii ya Marekani inaweza kusababisha kuongezeka tena kwa vita ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili zinazoshika nafasi mbili za mwanzo duniani kwa nguvu ya kiuchumi. Ripoti imemnukuu mtafiti mwandamizi wa Baraza la Mahusiano na Nje la Marekani Bw. Edward Alden akisema vita ya kibiashara inayofanywa na serikali ya sasa dhidi ya China imeshindwa, lakini bado inaendelea kutunga mkakati wa muda mrefu utakaoshindwa.

    Wakati huohuo vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo shirika la utangazaji la Marekani NBC vimefichua uwongo kuwa hasara zote zinazotokana na kuongezeka kwa ushuru zitabebwa na China, na kusema utafiti umeonyesha kuwa katika mwaka mmoja uliopita, wauzaji walikabidhi nyongeza ya ushuru wa bidhaa za China iliyotozwa kwa wateja kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, na kama raundi mpya ya nyongeza ya ushuru itatekelezwa, bei za bidhaa zinazotumiwa kila siku wanazohitaji raia wa Marekani zitazidi kuwa kubwa.

    Uchambuzi unasema kutishia kuongeza tena ushuru wa bidhaa za China kunakwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili walipokutana mjini Osaka, na kuashiria kuwa baadhi ya watu wa Marekani wanaendelea na mtazamo uliopitwa na wakati wa kunufaisha upande mmoja, ambao hakika utayapa changamoto majadiliano ya kibiashara kati ya China na Marekani, kuharibu maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na wa sehemu nyingine, na kuongeza hatari ya kuzorota kwa uchumi wa dunia. China siku zote inayapa kipaumbele majadiliano katika utatuzi wa mgogoro wa kibiashara kati yake na Marekani, lakini wakati huohuo imesema mara nyingi kuwa kama Marekani inataka vita, China itajibu mpaka mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako