• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uturuki asema nchi hiyo itafanya operesheni kaskazini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2019-08-05 09:40:23

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake itafanya operesheni ya kijeshi kaskazini mwa Syria dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi ambao wanawachukulia kama "tishio kubwa la kiusalama".

    Rais Erdogan amesema hayo mjini Bursa, kaskazini magharibi ya Uturuki kwenye hafla ya ufunguzi wa barabara, na kuongeza kuwa operesheni hiyo itakayofanyika mashariki ya mto Euphrates kaskazini mwa Syria, eneo linalodhibitiwa na kundi la YPG.

    Wiki mbili zilizopita, wajumbe wa kijeshi wa Marekani na Uturuki walifanya mazungumzo kuhusu kuanzishwa kwa eneo salama, lakini hawajafikia mwafaka.

    Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw. Mevlut Cavusoglu amesema, kutokana na hali hiyo, nchi yake italazimika kuanzisha eneo salama yenyewe bila ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako