• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni husika za China kusimamisha uagizaji mazao ya kilimo kutoka Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-06 09:20:12

    Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China na wizara ya biashara ya China zimesema, kutokana na Marekani kutangaza kuongeza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 300, ambayo ni kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili huko Osaka, Japan, kamati ya ushuru ya baraza la serikali ya China imeamua huenda ikaongeza ushuru kwa mazao ya kilimo ya Marekani baada ya tarehe 3 Agosti, na kampuni husika za China zimesimamisha kununua mazao hayo kutoka Marekani.

    Idara husika ya China imesema, soko la China ni kubwa, na lina mustakabali mzuri wa kununua mazao ya kilimo ya Marekani yenye ubora wa juu, lakini China inatumai Marekani itatekeleza makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili huko Osaka, kutimiza ahadi yake, na kutoa mazingira mazuri kwa ushirikiano wa kilimo kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako