• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Marekani watangaza majina ya watu waliouawa katika mauaji makubwa ya Texas

    (GMT+08:00) 2019-08-06 17:09:10

    Polisi wa mji wa El Paso wa jimbo la Texas nchini Marekani wametangaza majina ya watu waliouawa katika tukio la mauaji makubwa yaliyotokea tarehe 3, miongoni mwao kuna wageni wasiopungua wanane.

    Mkurugenzi wa idara ya polisi ya mji wa El Paso Bw. Greg Allen amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, kati ya watu 22 waliouawa, kuna wanaume 12 na wanawake 10, wakiwemo wamarekani 13, watu 7 kutoka Mexico na mjerumani 1, na majeruhi 9 wameruhusiwa kutoka hospitali, na wengine 15 bado wako hospitali.

    Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Mexico Bw. Marcelo Ebrard jana alisema Mexico itashiriki kwenye uchunguzi wa tukio hilo na kuitaka Marekani kuongeza ufuatiliaji dhidi ya ubaguzi wa rangi na umwamba wa wazungu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako