• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yatakiwa kuwema mazingira bora kwa uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-08-06 19:58:49

    Waziri wa Viwanda na Biashara, wa Tanzania Innocent Bashungwa, ametoa wito kwa nchi zote za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kutilia mkazo uboreshaji wa mazingira wezeshi na wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza katika viwanda.

    Alitoa rai hiyo jana wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC jijini Dar es Salaam, akiungwa mkono na Katibu Mtendaji wa jumuiya hiyo, Dk. Stergomena Tax na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Salum Shamte.

    Alibainisha kuwa mauzo ya Tanzania kwenda nchi za SADC kwa mwaka 2018 yalikuwa Dola za Marekani milioni 999 ikilinganishwa na Dola milioni 875 mwaka 2017.

    Alisema takwimu hizo zinaonyesha ongezeko la asilimia 12.16 na uingizaji wa bidhaa Tanzania kutoka SADC uliongezeka kutoka Dola milioni 600.64 mwaka 2017 hadi kufikia Dola milioni 604.32 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.61.

    Alitaja bidhaa muhimu ambazo Tanzania inauza SADC kuwa ni pamoja na madini mbalimbali kama vile tanzanite na dhahabu, bidhaa za kilimo kama vile chai na kahawa, bidhaa za viwandani kama vile plastiki, tumbaku, saruji, marumaru, dawa na vifaa tiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako