• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dereva Manvir Baryan aendeleza weledi wa Kenya katika Mbio za Magari barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-07 08:37:56

    Dereva Manvir Baryan ameendeleza weledi wa Kenya katika Mbio za Magari za barani Afrika baada ya kutwaa taji la mwaka 2019, wikendi. Baryan, ambaye aliibuka bingwa wa mashindano haya ya duru ya saba mwaka 2017 na 2018, alitetea taji lake baada ya kuandikisha ushindi wake wa tatu msimu huu aliponyakua taji la Pearl Rally nchini Uganda. Akishirikiana na mwelekezi wake Drew Sturrock kutoka Scotland, Baryan alishinda duru ya Pearl kwa urahisi. Katika gari lao la aina ya Skoda Fabia, walidhibiti duru ya Uganda kutoka mwanzo hadi mwisho. Baryan alifungua msimu kwa kutwaa taji la Bandama Rally nchini Ivory Coast mwezi Februari. Ushindi wake wa nchini Uganda umemfanya kuzoa alama 201 zikisalia duru mbili za mwisho zitakazofanyika nchini Tanzania mnamo Septemba 13-15 na Rwanda mnamo Oktoba 4-6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako