• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA-Tanzanite yachapwa 2-1 na Zambia COSAFA, kumenyana na Zimbabwe nusu fainali

    (GMT+08:00) 2019-08-07 08:38:21

    TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imepoteza mechi ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya kuchapwa 2-1 na Zambia jioni ya jana Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini. Katika mchezo huo wa mwisho wa Kundi B, mabao ya Zambia yamefungwa na Florence Kasonde dakika ya nne na Christine Kalenge dakika ya 61, wakati la Tanzania lilifungwa na Enekia Kasonga dakika ya 84. anzania sasa itamenyana na Zimbabwe kesho katika Nusu Fainali kuanzia Saa 5:00 asubuhi, wakati Zambia itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini kuanzia Saa 9:00 Alasiri. Jana Tanzania ilipoteza mechi ya kwanza baada ya mwanzo mzuri, ikishinda mechi zake zote mbili za mwanzo 2-0 dhidi ya Botswana na 8-0 dhidi ya Eswatini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako