• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZFF kuiweka kiti moto CAF

    (GMT+08:00) 2019-08-07 08:38:38

    Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Seif Kombo Pandu amesema anaandaa mpango, ili kuwaalika viongozi wa juu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa lengo la kujadili hatma ya Zanzibar juu ya kupata nafasi ya kuwa mwanachama kamili wa shirikisho hilo. Alisema viongozi hao wa CAF watakapokwenda watakaa na wanasheria ili kuweza kulijadili suala hilo na kupata muafaka. Alibainisha kuwa hivi karibuni alishiriki mkutano wa shirikisho hilo uliofanyika nchini Misri, ambapo kuna mafanikio makubwa wameweza kuyapata ikiwemo kuweza kuingiziwa mgao wao wa fedha ambao kwa kipindi kirefu haukuingizwa. Hata hivyo alisema katika kikao hicho walibaini kuwa Zanzibar ilipoingizwa kwenye uanachama wa CAF ilipigiwa kura na nchi nyingi, lakini wakati wa kutolewa ilitolewa kienyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako