• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wayne Rooney kumrithi Lampard Derby County 

    (GMT+08:00) 2019-08-07 08:38:59

    Nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney anajiunga na klabu ya Derby County mwezi Januari na kuwa kocha mchezaji wa timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza England. Rooney anakwenda kujaza nafasi ya Frank Lampard aliyerejea England kuinoa Chelsea. Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuachana na klabu yake ya DC United ya Ligi Kuu Marekani. Rooney amebakiza miezi 13 kabla ya mkataba wake wa miaka mitatu DC United kumalizika. Kwa mujibu wa taarifa, Rooney anatarajiwa kwenda kuanza kazi mpya Derby Januari, mwakani lakini huenda nguli huyo akakatiza mkataba mapema. Derby jana ilianza vyema Ligi Daraja la Kwanza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Huddersfield ikiwa chini ya kiungo wa kati wa zamani wa Uholanzi kocha Phillip Cocu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako