• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa Zambia na Rwanda wazindua kituo Kikuu cha Maendeleo Endelevu

  (GMT+08:00) 2019-08-07 19:17:21

  Rais wa Zambia Edgar Lungu na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wamezindua leo kituo Kikuu cha Maendeleo Endelevu cha (SDGs) kanda ya Kusini mwa Afrika.

  Uzinduzi huo umeleta pamoja zaidi ya maafisa 200 wa serikali, mashirika ya kimataifa, taasisi za maendeleo na wataalam kujadili masuala yanayohusu utekelezaji wa SDG Kusini mwa Afrika,

  Waziri wa Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa Alexander Chiteme wa Zambia, amesema uzinduzi huo unafuatia kusainiwa kwa makubaliano ya nchi mnamo Septemba 2018 kati ya serikali ya Zambia na Kituo cha SDG cha Afrika.

  Kituo hicho kikuu cha kikanda, kitasaidia nchi za kusini mwa Afrika kukabili vizuizi vya utekelezaji wa SDG na kusaidia kufikia malengo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako