• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Manara na wenzake watatu waburuzwa Mahakamani

    (GMT+08:00) 2019-08-08 08:59:25

    Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara na wenzake watatu wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Imeelezwa kuwa wanadaiwa deni na fidia ya Tsh. milioni 83.3 baada ya kupokea bidhaa zenye nembo ya Dela Boss Perfume bila kuzilipia. Mbali na fedha hizo, Mlalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Abu Masoud Al Jahdhamy, Ameiomba mahakama kuwaamuru washtakiwa hao watatu ambao ni, Haji Manara, Beatrice Ndungu na Palm General Supply kumlipa fidia nyingine itakayoona zinafaa ikiwemo gharama za mawakili. Kesi hiyo ya madai ilitajwa jana na kuahirishwa mpaka tarehe 29 Agosti Mwaka huu itakapotajwa tena. Katika madai ya msingi, mlalamikaji amefungua kesi hiyo akiwadai walalamikiwa fedha hizo baada ya kuwasambazia bidhaa zenye nembo ya "De La Boss Perfume" Tanzania na bidhaa hizo zimetengenezwa Dubai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako