• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yawasilisha barua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu vikwazo vipya vya Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-08 09:12:32

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Iran imewasilisha barua katika Baraza la Usalama la Umoja huo inayoutaka Umoja wa Mataifa kupinga vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani.

    Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Bw. Majid Takht Ravanchi amewasilisha barua hiyo kwa katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres, kumtaka kuipinga Marekani baada ya nchi hiyo kuweka vikwazo vipya dhidi ya waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif.

    Ameongeza kuwa Bw. Guterres ametoa wito kwa pande zote kuepuka hatua yoyote inayoweza kusababisha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi iliyopo sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako