• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watanzania wahimizwa kuchangamkia fursa za SADC

  (GMT+08:00) 2019-08-08 19:26:19

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukanda maalum wa Uwekezaji nchini Tanzania (EPZA) Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia,amesema Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ina fursa za uwekezaji na soko kubwa ambavyo kwa pamoja ni vitu muhimu katika maendeleo ya viwanda na juhudi za kuondoa umaskini.

  Akizungumza katika Maonyesho ya Nne ya Viwanda ya SADC yanayofanyika katika ukumbi wa kimtaifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana,Simbakalia alisema SADC imejaa fursa lukuki za uwekezaji zikiambatana na mtaji mkubwa wenye nguvu kazi ya vijana ambayo ni nguzo muhimu sana katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

  Alisema SADC inafaa itumie fursa ya uhusiano na China katika kujenga mikakati imara zaidi yenye lengo la kuleta maendeleo endelevu katika ukanda huo.

  Alisema ni vyema SADC kuelekeza nguvu katika uzalishaji wa bidhaa mpya na mitambo inayotumika sehemu mbalimbali za uzalishaji kwa kutumia aina mbalimbali za madini yanayopatikana katika nchi wanachama.

  Maonyesho ya Nne ya SADC ya Viwanda yalifunguliwa rasmi jumatatu na Rais Magufuli ambaye katika kilele cha Mkutano wa Jumuiya ya SADC atachukua wadhifa wa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako