• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa kundi la Houthi la Yemen wasema wamefanya shambulizi dhidi ya mnara wa kuongoza ndege nchini Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2019-08-09 09:33:34

    Waasi wa kundi la Houthi nchini Yemen wamesema wameshambulia mnara wa kuongoza ndege katika uwanja wa ndege wa Abha ulioko mkoa wa Asir, kusini magharibi mwa Saudi Arabia.

    Msemaji wa kundi hilo Yahya Sarea amenukuliwa na kituo cha televisheni cha kundi hilo al-Masirah akisema, waasi hao wamefanya mashambulizi mawili dhidi ya mnara huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani zilizokuwa na mabomu.

    Wakati huohuo, kituo cha Televisheni cha Saudi Arabia Al Arabiya kimesema, jeshi la anga la nchi hiyo lilizuia na kuangusha ndege isiyo na rubani iliyorushwa na wapiganaji wa kundi la Houthi jana usiku iliyokuwa ikielekea mkoa wa kusini magharibi wa Jizan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako