• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watoa wito wa kuchukua hatua kukabiliana na hatari ya uhaba wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2019-08-09 09:33:57

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Jopo la Maingiliano ya Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) ni sehemu nyingine ya ushahidi unaoelekeza kuwa hatua za dharura zinatakiwa kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Kutokana na ripoti hiyo, mabadiliko ya tabianchi yanaleta tishio kubwa kwa upatikanaji wa chakula duniani, na ingawa usimamizi mzuri wa ardhi unaweza kusaidia kukabiliana na kuongezeka kwa joto duniani, kupunguza utoaji wa hewa chafu katika sekta zote ni lazima ili kuzuia joto la dunia lisiongezeke kwa zaidi ya nyuzi 2.

    Amesema kuna hatua kadhaa za kiasili zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na uhaba wa chakula, na kwamba mkutano ujao wa kilele wa Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi utakuwa fursa muhimu ya kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako