• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI- Serena Williams apenya kiurahisi kwenye raundi ya tatu ya kombe la Rogers huko Toronto

    (GMT+08:00) 2019-08-09 09:42:11

    Serena Williams amepenya kiurahisi kwenye raundi ya tatu ya kombe la Rogers huko Toronto akimshinda Mbelgiji Elise Mertens. Bingwa huyo wa mara 23 wa Grand Slam mwenye miaka 37 alishinda seti 6-3 6-3 na kufanya wawe sare na Mrussia Ekaterina Alexandrova. Kwengineko Mjapani Naomi Osaka anazidi kujisogeza mbele ili kufikia tena nafasi yake ya namba moja duniani baada ya mpinzani wake Tatjana Maria kusalimu amri kwa seti 6-2. Kuangushwa kwake kwenye raundi ya pili na Ashleigh Barty kumemfanya akubali kuuachia utawala wake wa wiki nane akiwa namba moja duniani, huku Karolina Pliskova pia akingángána kufikia kileleni. Mczech Pliskova amemshinda Mmarekani Alison Riske kwa seti 6-4 6-7 na kufanya raundi ijayo akutane na Anett Kontaveit. Kwa upande wa bingwa mtetezi Simona Halep amemshinda Mmarekani Jennifer Brady kwa seti 4-6 7-5 7-6, huku Elina Svitolina bingwa wa mwaka 2017 akimshinda Katerina Siniakova 6-3 3-6 6-3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako