• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UHAMISHO- Wachezaji waliohamishwa na waliokosa uhamisho

    (GMT+08:00) 2019-08-09 09:43:35

    Likiwa dirisha la uhamisho sasa limeshafungwa rasmi kuna wachezaji waliopenda kwenye dirisha hilo na pia kuna wale waliokwama na kusalia kwenye timu zao. Mshambuliaji wa klabu ya Genk nchini Ubelgiji na nahodha wa timu ya taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta amekosa kujiunga na klabu ya England baada ya dirisha la uhamisho la taifa hilo kufungwa rasmi. Samatta ambaye kulingana na gazeti la The Sun la England ana thamani ya pauni milioni 12 bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa. Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley. Nayo Tottenham imethibitisha kumsajili kiungo wa kati Giovani Lo Celso kutoka klabu ya Uhispania ya Real Betis kwa mkopo wa muda mrefu kukiwa na uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa kudumu. Kwa upande wa Mshambuliaji wa zamani wa England Andy Carroll amerudi katika klabu yake ya utotoni miaka minane baada ya kuondoka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, aliachiliwa na kuwa mchezaji huru na klabu ya West Ham msimu huu. Na Inter Milan wametuma ujumbe wa twitter ulio na kanda ya video ya Lukaku akiwa amevalia jezi ya timu hiyo akisema ''Inter sio ya kila mtu ndio sababu niko hapa'' Romelu Lukaku amesaini mkataba hadi tarehe 30 Juni 2024. Lukaku sasa atakuwa mchezaji wa tatu aliye ghali zaidi kusajiliwa na ligi ya Serie A kufuatia uhamisho huo wa dau la pauni milioni 74.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako