• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa bwawa Kariminu wang'oa nanga

    (GMT+08:00) 2019-08-09 18:30:20

    Mradi mkubwa wa maji wa Kariminu II Dam nchini Kenya wa kiasi cha Sh24 bilioni katika maeneo ya Buchana, Kiriko, Gathanji na Kanyoni tayari umeanza kuchimbwa.

    Matingatinga yalifika katika maeneo hayo mwishoni mwa wiki jana ambapo kufikia sasa kazi inaonekana ikiendelea kwa kasi.

    Wakazi wa sehemu ya kwanza ya Kariminu I Dam walilipwa fidia zao huku wale wa sehemu ya pili wakiwa wanakaribia kukamilishiwa haki yao.

    Mbunge wa Gatundu Kaskazini Bi Wanjiku Kibe tayari amewahakikishia wakazi hao wawe na subira huku matakwa yao yakishughulikiwa haraka iwezekanavyo.

    Wakazi wa Kanyoni na Gathanje wanaitaka serikali iharakishe fidia katika kikundi cha pili kwa sababu wanataka kujitafutia ardhi kwingineko.

    Hivi majuzi Waziri wa Maji Bw Simon Chelungui alizuru sehemu hiyo na kujionea mwenyewe jinsi kazi hiyo ilivyotarajiwa kuzinduliwa rasmi.

    Sehemu ya kwanza ya eneo hilo ni ya ekari 171.6 ambako zinatoka familia 246. Tayari zimeshapokea takribani Sh1.28 bilioni kama fidia.

    Kulingana na wahandisi wa mradi huo, bwawa hilo ni la futi 59 na linatarajiwa kusambaza maji mengi kwa takribani watu milioni moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako