• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Afrika Kusini kununua hisa Vodacom

  (GMT+08:00) 2019-08-09 18:42:15

  Mamlaka za usimamizi nchini Tanzania zimetoa vibali vyote vinavyohitajika kwa ajili ya mauzo ya hisa za kampuni ya huduma za simu ya Vodacom Tanzania, hatua ambayo itaifanya kampuni mama ya Vodacom Group kuweza kumiliki hadi asilimia 75.

  Novemba mwaka jana wanahisa wa Vodacom Tanzania waliidhinisha kuuzwa kwa asilimia 26.25 ya hisa zake kwa kampuni ya Vodacom Group zilizokuwa zikimilikiwa na kampuni ya Mirambo Limited.

  Vodacom Group ya Afrika Kusini, ambayo kwa sasa inamiliki asilimia 61.6 ya hisa za Vodacom Tanzania, itaongeza umiliki wake baada ya kununua hisa milioni 588 za Mirambo Limited kwa gharama ya Sh499.8 bilioni.

  Mirambo itapata Sh850 kwa kila hisa moja ambayo ni kubwa kuliko bei ya sasa ambayo ni Sh800 kwa hisa moja. Bei inayotolewa na Mirambo kwa Vodacom Group ni sawa na ile ya mauzo ya awali kwa umma (IPO).

  Kwa mujibu wa taarifa ya Vodacom Group ambayo imeorodheshwa katika soko la hisa la Johannesburg, idhini ya maombi ya muamala huo imetolewa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Tume ya Ushindani (FCC) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako