• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya China kinaendana na misingi ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2019-08-10 17:36:42

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya China (REER) cha mwaka jana, kiliendelea kuwa kama ilivyoagizwa na kuwa sawa na sera zinazotakiwa za IMF.

    Ripoti ya IMF imesema baada ya kufanya mapitio ya uchumi wa China, kiwango cha ubadilishaji wa sarafu ya China kiliongezeka kwa asilimia 1.4 ikilinganishwa na mwaka jana.

    Mchumi na mshauri wa Umoja wa Mataifa Bw Jeffrey Sachs, amesema IMF imesema wazi kuwa China haifanyii ujanja sarafu yake na kuwa urari wa biashara na nje wa China unafaa.

    Akizungumzia uamuzi wa wizara ya fedha ya Marekani kuitaja China kuwa nchi inayoifanyia ujanja sarafu yake, Bw. Sachs amesema uamuzi huo ni mbaya, una hila na ni wa kisasa, ambao msingi wake ni mambo anayoandika Rais Trump kwenye Twitter, na sio uchambuzi wa kina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako