• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia itafanya hatua kamili kulinda usalama wa taifa

    (GMT+08:00) 2019-08-10 17:51:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Russia Bi. Maria Zakharova amesema kutokana na maagizo ya rais Vladmir Putin wa Russia, wizara hiyo itashirikiana na ofisi nyingine za serikali kufuatilia hatua za Marekani katika uendelezaji, utengenezaji na uwekaji wa makombora ya masafa ya kati na mafupi, na Russia itajibu wakati Marekani inachukua hatua hizo ili kulinda usalama wake.

    Bi. Zakharova amesema hayo mjini Moscow kwenye mkutano wa waandishi wa habari. Pia amesema Russia inatoa wito kwa Marekani na washirika wake kutimiza wajibu wa kushiriki kwenye pendekezo la Russia la kusitisha kuweka makombora husika, na Russia ina nia ya kufanya mazungumzo yenye usawa na ya kiujenzi na Marekani kuhusu makubaliano ya makombora ya masafa ya kati na masuala mengine ya utulivu wa kimkakati katika msingi wa kuheshimiana na kujali maslahi ya upande mwingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako