• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KMKM yaanzia kushoto Ligi ya Mabingwa Afrika

  (GMT+08:00) 2019-08-12 08:50:18
  Wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, KMKM imeanza vibaya kampeni hizo baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 mbele ya Club Desportivo De Agosto kwenye uwanja wa Amaan. Ikicheza mbele ya mashabiki kiasi waliohudhuria mchezo huo, KMKM ilishindwa kuzitumia nafasi chache walizozipata huku wageni wakionekana kutawala uwanja na kuwaweka wanamaji hao kwenye wakati mgumu. Agosto walianza kuziona nyavu za KMKM kwenye dakika ya 71 kupitia goli lililofungwa na Manuel David kabla ya Lionel Yombi kuongeza goli la pili kunako dakika ya 89. Magoli hayo yalitosha kuichanganya KMKM na kujikuta wakicheza bila ya umakini na kuwaruhusu wapinzani wao kutawala mchezo.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako