• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Samatta yapoteza tena

  (GMT+08:00) 2019-08-12 08:52:48
  Mabingwa watetezi, KRC Genk juzi wamepoteza mechi ya pili mfululizo ya Ligi daraja la Kwanza A Ubelgiji, baada ya kuchapwa 2-0 nyumbani na Zulte-Waregem uwanja wa Luminus mjini Genk. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mfungaji bora wa timu hiyo msimu uliopita, Mbwana Samatta alicheza kwa dakika zote 90 lakini kwa mara nyingine akashindwa kufunga. Katika mechi ya kwanza ya Ligi hiyo, Genk ilichapwa 3-1 na wenyeji, KV Mechelen Agoti 3 uwanja wa AFAS mjini Mechelen, Malines siku ambayo Samatta alifunga bao lake la kwanza la msimu katika dakika ya 45, akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako